Home BENKI Joint Account: Faida na hasara zake

Joint Account: Faida na hasara zake

0 comment 108 views

Akaunti za pamoja maarufu kama ‘Joint Account’ hufunguliwa mara nyingi na wanandoa, ndugu wa karibu, washirika katika biashara, washirika wa nyumbani au watu ambao wanaona kuna umuhimu wa kushirikiana na majukumu ya usimamizi wa fedha. Kawaida, pande zote mbili huwa na mamlaka ya kuendesha akaunti kulingana na makubaliano yanayofanywa wakati wa kufungua akaunti.

Kuwa na akaunti ya pamoja kunahitaji uaminifu katika pande zote zinazohusika.

Hizi ni baadhi ya faida na hasara za kufungua akaunti  ya pamoja

Faida

  • Ni rahisi kwa pande zote kufikia fedha ikiwa pande moja haiwezi kufikia fedha kwa haraka au wakati wa uhitaji kwa mfano kama mmoja wapo kasafiri, amefariki nk ni rahisi kwa pande nyingine kuzifikia fedha katika akaunti ya pamoja. Mara nyingi akaunti binafsi hufungwa ikiwa mmiliki wa akaunti husika hayupo wakati wa kufanya muamala lakini kwa akaunti ya pamoja mtu aliyekuwepo katika akaunti ya pamoja huruhusiwa kufanya miamala,.
  • Kuwa na akaunti ya pamoja husaidia kujua matumizi ya fedha ya kila mshiriki katika akaunti husika. Kwa kujua hilo inakuwa rahisi kuona matumizi.
  • Usimamizi wa akaunti hii ni rahisi hivyo ni rahisi kwa pande zote kupata huduma mbalimbali.
  • Akaunti ya pamoja huongeza uaminifu kwa sababu kwa kujua hali ya kifedha katika pande zote basi kila mmoja ataona hakuna sababu ya kuwa na siri.
  • Kuwa na akaunti ya pamoja hurahisisha kujua mapato na matumizi na kusaidia kupanga mipango ya baadae.

Hasara

  • Ikiwa kutatokea changamoto baina ya pande zilizofungua akaunti basi kuna nafasi kubwa ya kuwa na ugomvi/vurugu.
  • Kuwa na akaunti ya pamoja hupoteza faragha kwani kila muamala utakavyofanywa basi pande ambayo haijafanya muamala itajulishwa kuwa muamala umefanyika.
  • Akaunti ya pamoja husababisha pande ambayo haiwekezi fedha nyingi kuwa tegemezi kwa upande unaowekeza fedha nyingi zaidi.
  • Kwa namna moja au nyingine usalama wa fedha katika akaunti ya pamoja huwa si 100% kwa sababu mmoja wa wamiliki wa akaunti ya pamoja ana uwezo wa kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuathiri pande nyingine.

Kuwa na akaunti ya pamoja sio jambo baya hasa kwa watu wa karibu wanaoshirikiana kwenye majukumu mbalimbali. Ili kuepuka changamoto inashauriwa kuwa na akaunti binafsi ambayo itakuwezesha kufanya miamala kwa uhuru na faragha zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter