Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Hospitali yasaidia wagonjwa kuwa wajasiriamali

Hospitali yasaidia wagonjwa kuwa wajasiriamali

0 comment 134 views

 

Na Mwandishi wetu

Hospitali ya Afya ya Akili iliyopo Korogwe mkoani Tanga imekuwa inawasaidia baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya wanaopelekwa katika hospitali hiyo kwa kuwafundisha namna ya kutengeneza samani kama viti vya nyumbani na hotelini pamoja na kapeti ili kuwaandaa kuwa wajasiriamali pindi watakapomaliza matibabu yao.

Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo, Amina Ramadhani amesema baada ya kupokea wagonjwa hawa, wanakaa nao kwa kipindi fulani na wakionyesha maendeleo mazuri kiafya, wanapatiwa elimu ya ufundi wa kutengeneza samani ambayo wengi wamekuwa wakifanya vizuri. Hii inawasaidia kutumia muda wao vizuri badala ya kukaa bila kazi.

Fursa hii wanayopewa wagonjwa inawasaidia kuondokana na utegemezi mara baada ya kupona kwani wanakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kujiingizia kipato kutokana na bidhaa wanazotengeneza ambazo soko lake kubwa ni Wilaya ya Bagamoyo

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter