Home AJIRA Waajiri wasiotekeleza Sheria ya watu wenye ulemavu wapewa onyo

Waajiri wasiotekeleza Sheria ya watu wenye ulemavu wapewa onyo

0 comment 136 views

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Stella Ikupa amewataka waajiri hapa nchini kutekeleza Sheria ya watu wenye ulemavu na kuwapatia ajira na kuonya kuwa watachukuliwa hatua vinginevyo. Ikupa amesema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua mkutano wa waajiri kuhusu ajira kwa watu walio na ulemavu uliondaliwa na uongozi wa hospitali ya CCBRT.

“Ninawataka waajiri kutekeleza Sheria ya Watu wenye Ulemavu No. 9 ya mwaka 2010 kifungu cha 31 kinachomtaka kila mwajiri mwenye zaidi ya waajiri 20 kuhakikisha asilimia tatu ya waajiri hao ni watu wenye ulemavu. Wengine wamediriki hata kutoa vigezo ambavyo havina sababu za msingi kwa kusema hawana kazi za kuwafaa watu wenye ulemavu. Hawa waajiri nawataka kuachana na mtazamo hasi. Watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa katika utendaji kazi, hivyo msiwabague”. Amesema Naibu waziri huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi amesema wameandaa mkutano huo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika 3 Desemba kila mwaka. Mkurugenzi huyo amesema kuwa lengo kubwa la warsha hiyo ni kuongeza uelewa wa waajiri kuhusu haki za watu wenye ulemavu katika soko la ajira.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter