Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche amesema benki hiyo imejipanga kutoa mikopo kwa vikundi maalum vikiwemo Vicoba na Saccos kwa mwaka 2019 ambapo vikundi mbalimbali vimekuwa vikipewa mafunzo na maafisa ustawi wa jamii ili kuweza kunufaika na mikopo hiyo kwa kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na kuinua uchumi wao na wa taifa kwa ujumla. Nyambuche ameeleza kuwa Banc ABC imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii na wamekuwa wakiwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao.
“Tuna mawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo”. Amesema Nyambuche.
Banc ABC nchini imekuwa ikiwekeza katika jitihada mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo. Benki hiyo imefanya hivyo kwa jamii ya kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii hapa nchini. Aidha, Banc ABC imeendelea kushirikiana na serikali ili kuchochea maendeleo ya jamii kwa kutumia dhana ya uwezeshaji wa mikopo yenye masharti nafuu.