Home BENKI CRDB, VISA waleta mfumo mpya wa malipo

CRDB, VISA waleta mfumo mpya wa malipo

0 comment 90 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei amesema wanashirikianana kampuni ya Visa ili kutoa huduma zake kwa kutumia simu za mkononi (mVisa). Dk. Kimei ameeleza kuwa wao kama taasisi ya kifedha watendelea kuwa wabunifu ili kukabiliana na mahitaji ya wateja wao ambayo amedai yanabadilika siku hadi siku kutokana na ukuaji wa teknolojia.

Programu hiyo itakayozinduliwa hivi karibuni itawezesha wateja wa benki hiyo kufanya malipo kwa kutumia simu za mkononi popote dunianiVilevile, uzinduzi wa program hiyo utawapa fursa wateja kufanikisha malipo ya aina mbalimbali pasipo kubeba fedha taslimu wala kadi za benki (ATM)

Hivi sasa benki ya CRDB ina matawi zaidi ya 250 nchi nzima pamoja na vituo vya mauzo (PoS) na mawakala. Kimataifa benki hiyo kupitia kadi za mkopo, inafanikisha miamala mbalimbali na kutoa fursa ya kukopa hadi Sh. 100 milioni kwa njia ya mtandao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter