Home BENKI CRDB yamtangaza bosi mpya

CRDB yamtangaza bosi mpya

0 comment 107 views

Benki ya CRDB kupitia bodi ya benki hiyo imemteua na kumtangaza Abdulmajid Musa Nsekela kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki akirithi nafasi ya Dk Charles Kimea kuanzia june 2018.

Nsekela ambaye safari yake ya kibenki ilianzia katika benki hiyo kabla ya kuondoka na kujiunga na benki ya NMB yapata muongo mmoja uliopita ana ufahamu wa kutosha kuhusu usimamizi na uongozaji wa taasisi za fedha huku akichagizwa na uzoefu na ubunifu wa bidhaa na huduma za kibenki kwa muda mrefu.

Nsekela mwenye uzoefu wa takribani miaka 20 katika huduma za kibenki anachukua nafasi ya mkurugenzi aliyeiongoza benki hiyo kwa mafanikio kwa kipindi cha miaka 21, Dk Charles Kimei ambae taarifa zinadai ameomba kupumzika na atastaafu rasmi ifikapo mei 2019.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Ally Laay, inamtaja Nsenkela kuwa alijiunga na benki hiyo kama afisa wa kawaida mwaka 1997 na miaka mitatu baadae akapandishwa kuwa meneja uhusiano ambapo ilimchukua miaka mitatu tena kupewa cheo cha Meneja Uhusiano Mwandamizi hadi hapo anaondoka na kujiunga na benki mpinzani kibiashara wa CRDB yaani NMB.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter