Home BENKI Exim kuinunua UBL

Exim kuinunua UBL

0 comment 113 views

Benki ya Exim imesaini barua, kama ishara ya nia yake kuinunua benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) iliyo chini ya wapakistani kwa asilimia 100, yaani mali na vilevile madeni. Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Exim, Jaffari Matundu, amesema lengo la kununua benki hiyo ni kujiimarisha, na kuzidi kujitanua kibiashara ndani na nJe ya nchi. Kwa mujibu wa taarifa, benki ya Exim ipo kwenye orodha ya benki tano kubwa nchini.

“Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka benki ya UBL”. Amesema Matundu

Aidha, Naibu huyo amewakaribisha wateja kutoka benki ya UBL na kuwataka kuchangamkia fursa zinazotolewa katika matawi ya benki ya Exim. Matundu ameongeza kuwa anaamini wafanyakazi wa UBL wataongeza nguvu ya utendaji kazi na kwa ushirikano baina yao na wafanyakazi wa Exim biashara na maendeleo katika benki hiyo itazidi kukua.

Kwa upande wake Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBL ,Gasper Njuu, amesema kuwa makubaliano kati ya benki hizo yameshafanywa huku taratibu na Sheria zinazohusisha ununuzi huo zinaendelea. Manunuzi hayo yanategemea kukamilika katikati ya mwaka huu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter