Home BIASHARA Mavunde: Total ni mfano wa kuigwa

Mavunde: Total ni mfano wa kuigwa

0 comment 92 views

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu) Anthony Mavunde. ametoa pongezi kwa kampuni ya Total Tanzania kwa harakati zake za kusaidia vijana walio na mawazo mazuri ya biashara na kutoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo. Mavunde amesema hayo jijini Dar es salaam katika hafla ya kutangaza washindi wa shindano la “Total start upper of the year” na kusema kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kuchochea maendeleo ikiwemo kuwawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia mafunzo na mitaji.

Katika maelezo yake, Mavunde amesema kuwa Total Tanzania imekuwa ikiwajengea uwezo watanzania ili waweze kujiletea maendeleo na hivyo kuinua maendeleo ya taifa kwa ujumla. Naibu huyo amesema serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu na kwamba ushirikiano na sekta binafsi ni muhimu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania, Tarik Moufaddal amesema kampuni hiyo inalenga kuwa mshirika wa kuleta maendeleo hapa nchini huku akisisitiza kuwa kampuni hiyo imepanga makubwa kwa watanzania katika kuchangia maendeleo.

Katika hafla hiyo, washindi watatu wa mwanzo walipatiwa tuzo pamoja na fedha taslimu Sh. 75 milioni.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter