Home BENKI NMB yazindua huduma ya KLik

NMB yazindua huduma ya KLik

0 comment 85 views

Ni jambo ambalo linaonekana kuwa geni miongoni mwa watanzania, lakini ndio uhalisia. Benki ya NMB imezindua huduma mpya itakayomwezesha mteja kufungua akaunti ya benki kwa kutumia simu akiwa mahali popote. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Uvumbuzi wa Benki ya NMB, Joseph Njambi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo iliyopewa jina la KLik.

Njambi amesema huduma hiyo imekuja kuleta mapinduzi katika sekta ya benki na kudai kuwa itasaidia kuboresha utoaji wa huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma za malipo.

“Sasa unaweza kufungua akaunti popote ulipo bila kujaza fomu na hakuna malipo wala makato yoyote. Pia huna haja tena ya kwenda kupanga foleni kwenye tawi ili upate huduma”. Amesema Njambi.

Akieleza namna huduma hiyo itakavyokuwa ikifanya kazi, Njambi alisema mteja atatumia namba ya akaunti kwa watumiaji wa simu za smartphone na za kawaida.

“Faida nyingine hakuna kianzio wala makato ya mwezi, baada ya kufungua akaunti utatumia chini ya dakika tatu mteja utapokea faida ya asilimia tano hapo hapo ambayo itakokotolewa kwa mwaka kulingana na kiasi cha fedha” Alisema.

Soma Pia NMB yamwaga mabilioni kwa serikali

Njambi amedai kuwa huduma hiyo itaambatana na programu ya simu ambayo itasaidia watumiaji kufanya malipo ya bili  pamoja na kukokotoa thamani ya fedha. Akizungumzia kuhusu ujio wa huduma ya KLik, Mkurugenzi wa NMB Ineke Bussemaker amesema huduma hiyo imeletwa mahususi ili kuendana na kasi ya ukuaji na maendeleo ya teknolojia ili kurahisisha huduma kwa wateja.

“Idadi ya watumiaji wa simu kwa Tanzania ni wengi na kupitia huduma hii ya KLik tutaweza kuwafikia wengi zaidi hasa maeneo ambayo hayana huduma za benki”. Ameeleza Bussemaker.

Soma Pia Ukiukaji wa masharti waiponza NMB

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Benard Kibesse akizindua huduma hiyo, ameipongeza benki ya NMB kwa kuanzisha huduma hiyo ya kimtandao na kuongeza kuwa ilikuwa ni moja ya ndoto zake kuona benki za kitanzania zikitoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao.

“Hakika hii ni hatua nzuri na inarandana na mipango ya kiuchumi ya nchi kuongeza matumizi ya kimtandao katika huduma za fedha”. Amesema Dk. Kibesse.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter