Home BENKI Walioajiriwa benki kuchunguzwa

Walioajiriwa benki kuchunguzwa

0 comment 90 views

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango ameagiza benki zote nchini kufanya uchunguzi wa wafanyakazi wao na kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuwa sio waaminifu ili kuwajengea wateja imani na benki zao. Dk. Mpango ameeleza lengo la kufanya hivyo kuwa ni kuwahakikishia wateja imani kutokana na idadi ya matukio ya uporaji wa fedha mara baada ya kutoka benki kungezeka. Waziri huyo pia ameagiza jeshi la polisi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanachunguza matukio ya uhalifu yanayotokea benki na kutaka hatua zichukuliwe endapo itagundulika wafanyakazi wa benki wanahusika katika matukio ya wizi.

 

Dk. Mpango amesisitiza kuwa chanzo cha matukio ya uhalifu mara baada ya kutoka benki ni wafanyakazi wasio waadilifu hivyo ili kufuta kabisa matukio hayo, ni lazima wake kuchunguzwa. Waziri huyo pia ameonya kuwa, viongozi wa benki itakayokaidi agizo hilo watawajibishwa endapo tukio la uhalifu likitokea.

 

Mbali na maagizo hayo, Dk. Mpango ametoa wito kwa wananchi kuepuka kukopa kupitia taasisi za fedha zenye riba kubwa na kwa dhamana ya mali kwani kufanya hivyo ni hatari kwa mali zao na badala yake ameshauri wawe na nidhamu ya fedha za mikopo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter