Home BIASHARA Biashara na Familia: Unachotakiwa kuzingatia

Biashara na Familia: Unachotakiwa kuzingatia

0 comment 118 views

Mara nyingi inatokea kuwa mtu anakuwa na wazo la biashara lakini anashindwa kuliendeleza kutokana na kukosa fedha. Wafanyabiashara na wajasiriamali wamekuwa wakipata wakati mgumu wanapojaribu kuomba mikopo benki au hata katika taasisi nyingine za fedha kwani wengi wao hawakidhi vigezo vinavyotakiwa.

Hali hii hupelekea wengi kuomba msaada kwa familia na marafiki wa karibu. Japokuwa ni rahisi zaidi kufanya hivyo, kuchanganya biashara na familia wakati mwingine huwa ni chanzo cha matatizo.

Ikiwa wewe unafikiria kuomba fedha kwa familia ili kuwezesha biashara yako, ni vizuri kuzingatia mambo haya muhimu:

  1. Ni muhimu kuwachukulia ndugu au marafiki ambao wameweka fedha zao katika biashara yako kama wawekezaji wengine hivyo hakikisha unachukua fedha hizo katika mfumo rasmi badala ya kuendesha mambo kiholela kwa kuwa mnafahamiana. Ikiwezekana andaa mkataba ambao utaeleza vizuri makubaliano yenu na kutambulika kisheria.
  2. Tafuta mwanasheria. Kabla ya kukubali fedha au mali ya aina yoyote ni muhimu kuomba ushauri kutoka kwa mwanasheria. Hii itakusaidia kujua muelekeo halisi wa biashara yako hata kama ikitokea mkishindwa kuelewana baadae. Badala ya kufanya mambo kwa kujuana ni vizuri kujua haki zako za msingi kwa mujibu wa sheria ili kulinda biashara yako.
  3. Kumbuka kuwa mtu akikupatia mkopo, unachotakiwa ni kulipa na riba. Mtu/watu hao hawana mamlaka ya kukwambia namna gani unapaswa kuendesha biashara yako wala kufanya uamuzi wowote. Hii ni changamoto kubwa hususani kama unashirikiana na familia yako. Hakikisha mnaelewana katika hili tangu mwanzo wa makubaliano.

Biashara ni ndoto wa watu wengi, hususani vijana lakini wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kutokana na kukosa mapato ya kujiendesha. Kama unaweza kuomba msaada katika familia yako kwenye hili fanya hivyo lakini zingatia misingi ya hapo juu ili kuepuka ugomvi na ndugu au marafiki wa karibu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter