Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Vitambulisho vyaingiza mabilioni TRA

Vitambulisho vyaingiza mabilioni TRA

0 comment 138 views

Kufuatia ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali 1,022,178 nchi nzima, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, amesema kiasi cha fedha Sh. bilioni 20.3 kimefikishwa katika mfumo wa malipo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Waziri Jafo amesema hayo wakati akizungumza na wakuu wa mikoa kabla ya kupitisha tathmini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali na kuongeza kuwa, wajasiriamali nchini wameweza kuchangia Sh. bilioni 20.44 ambapo kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 20.3 zimefanikiwa kuingizwa katika mfumo wa TRA na Sh. milioni  135.6 zipo mikononi mwa wakusanyaji.

“Mpaka kufikia Aprili 30, mwaka huu kiasi cha shilingi milioni 942.47 zilikuwa hazijaingia katika mfumo wa mapato wa TRA, lakini nashukuru ndani ya siku mbili hizi tatu wakuu wa mikoa wameweza kuzifikisha kwenye mfumo fedha nyingi zaidi, niwapongeze kwa hilo. Nitumie fursa hii kuwahimiza wakuu wa mikoa na watendaji ambao wamekusanya fedha za vitambulisho vya wajasiriamali na kutoziingiza kwenye mfumo wa malipo wa TRA kufanya hivyo mara moja”. Amesema.

Waziri huyo ameeleza kuwa lengo la Rais Magufuli ni kuhakikisha wajasiriamali wanaondokana na adha walizokuwa wanazipata hususani kutoka kwa  maaskari wa jiji, kwani wajasiriamali ni kundi linalochangia katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa awamu ya kwanza na ya pili, vitambulisho 1,850,000 vyenye thamani ya Sh. bilioni 37 vimetolewa na hadi Aprili 30, vitambulisho 1,022,178 vyenye thamani ya Sh. bilioni 20.44 vimetolewa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter