Home BIASHARA Msamaha wa riba wajaza wafanyabiashara TRA

Msamaha wa riba wajaza wafanyabiashara TRA

0 comment 93 views

Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfred Mregi amesema kuna uwezekano mkubwa wa kufikia malengo kutokana na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara kulipa riba ya msamaha wa kodi na adhabu kwenye malimbikizo ya nyuma. Mregi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa semina kwa wafanyabiashara wakubwa na kuongeza kuwa, ili taifa liendelee ni lazima vyanzo vya ndani kutumika huku akisisitiza kuwa kodi ndio chanzo kikuu.

“Tumeona wafanyabiashara wetu wengi wanapungukiwa na uelewa, kwenye semina hii tutawaelekeza utaratibu wa kuleta maombi, sifa zinazostahili ili mtu apewe msamaha na muda uliowekwa kisheria itawafanya wajitokeze kwa wingi kuleta maombi yatakayosikilizwa na kutolewa uamuzi”. Ameeleza Mregi.

Katika maelezo yake, Kamishna huyo amefafanua kuwa mabadiliko hayo katika sheria yanalenga kukusanya kiasi cha Sh. 500 bilioni ndani ya miezi sita. Marekebisho ya sheria hiyo kwa sasa yanampa nguvu Kamishna Mkuu wa TRA kusamehe riba na adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa asilimia mia moja lengo likiwa ni kuwasaidia wafanyabiashara pamoja na walipakodi kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter