Home BIASHARA Soko la Kariakoo kufunguliwa mwezi Agosti

Soko la Kariakoo kufunguliwa mwezi Agosti

0 comment 159 views

Shirika la Masoko ya Kariakoo limetangaza kurejeshwa kwa wafanyabiashara 891 sokoni Kariakoo baada ya ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa soko kuu kukamilika.

Taarifa ya Manejimenti ya Masoko ya Kariakoo inaeleza kuwa orodha hiyo ina majina ya wafanyabiashara waliokidhi sifa na vigezo.

“Wafanyabiashara wanaodaiwa na Shirika ambao wapo kwenye orodha wanajulishwa kuwa hawatarejeshwa sokoni hadi watakapolipa madeni ya kodi waliyolimbikiza kwa muda mrefu,” inaeleza taarifa hiyo.

Aidha, taarifa imeeleza kuwa Shirika linatoa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Julai 10 hadi Agosti 08, 2024 kwa wadaiwa wote kukamilisha malipo ya madeni huku kwa wale wenye hoja au maoni kuhusu majina yao kutoonekana kwenye orodha ya uhakiki wakipewa muda wa siku tatu kuanzia Julai 11 hadi 13 kuwasilisha madai yao.

Soma: Rais Dkt. Samia aagiza biashara saa 24 soko la Kariakoo

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter