Home BIASHARAUWEKEZAJI JPM awajia juu wapora ardhi

JPM awajia juu wapora ardhi

0 comment 59 views

Rais John Magufuli amekemea tabia ya matajiri kupora ardhi za wanyonge na kusingizia ni kwa ajili ya shughuli za uwekezaji au kuwa na leseni za uchimbaji madini na kuwaonya wasifanye hivyo hadi atakapomaliza awamu yake. Rais Magufuli amesema hayo katika ziara yake wilayani Bunda mkoani Mara, akisisitiza uporaji ardhi za wanyonge hautafanywa wakati wa utawala wake kwani enzi za utumwa zilikoma mwaka 1961 baada ya ukombozi wa nchi chini ya baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Katika utawala wangu sitaki kuona mwananchi maskini anadhulumiwa ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji, hii ndiyo serikali yangu, wasubiri niondoke ndio warudi kama walivyokuwa wamezoea”. Amesema Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli imetokana na malalamiko ya wananchi wa wilaya hiyo waliokuwa na mabango yakitaja jina la Magoma ambapo baada ya kuhoji, Rais alifahamishwa kuwa ni muwekezaji aliyepora ardhi bila kulipa wananchi wa eneo husika fidia.

“Ni lazima tuwe na utaratibu mzuri wa kuchukua ardhi za masikini, huwezi ukamtoa masikini ukamwambia hama, eti kwa sababu ana prospectus license ya wizara ya madini. Amekuta watu hapa ni lazima kama anataka kuwahamisha awalipe kwa fedha ninazotaka mimi na hii ni kwa mujibu wa Sheria na sio kuja kuwavuruga watu tu hapa eti kwa sababu una leseni ya ardhini ni lazima Sheria ya madini iende sambamba na Sheria za ardhi namba nne na ile ya vijiji Kifungu G”. Amesisitiza Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter