Home BIASHARAUWEKEZAJI JPM kufanya ziara, kuzindua miradi Mtwara

JPM kufanya ziara, kuzindua miradi Mtwara

0 comment 116 views

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara mkoani humo ambapo atazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Byanakwa amewaambia waandishi wa habari kuwa katika ziara hiyo itakayoanza tarehe 02 hadi 04 Aprili 2019, Rais Magufuli mbali na kuweka mawe ya msingi pia atazindua rasmi kituo cha afya cha Mbonde na vilevile barabara za Mangaka-Mtambaswala na Mangaka-Nakapanya zilizojengwa kwa kiwango cha lami.

“Miradi inayozinduliwa ni mikubwa ambayo itasaidia kuchochea kukua kwa uchumi wa Mtwara na kwa uchumi wa Mtwara na nchi kwa ujumla na pia ni miradi ambayo kwa Mtwara ina tija kubwa sana, hivyo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika maeneo yote yenye miradi ya maendeleo itakayozinduliwa ili kumsikiliza Mh. Rais”. Amesema Mkuu huyo wa Mtwara.

Rais Magufuli anatarajia kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata, kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin pamoja na Chuo cha Ualimu Kitangali. Hii inakuwa ziara ya pili ya Rais Magufuli mkoani Mtwara tangu mwaka 2015.

“Ujio huu wa Mheshimiwa Rais Magufuli ni fursa ya upendeleo mkubwa kwa mkoa wetu na wana-Mtwara kwa ujumla kwani hii ni mara ya pili Mheshimiwa Rais kutembelea mkoa wetu wa Mtwara”. Ameeleza Byanakwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter