Home BIASHARAUWEKEZAJI Majaliwa afurahia uwekezaji Mkinga

Majaliwa afurahia uwekezaji Mkinga

0 comment 87 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua mbalimbali za uwekezaji katika kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga baada ya kutembelea eneo la mradi wa viwanda 11 ikiwemo kiwanda saruji cha Hengya, kiwanda cha vioo, kiwanda cha vifaa vya kisasa vya ujenzi, uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wilayani Mkinga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa, uwekezaji huo utaleta manufaa makubwa kwa taifa na wananchi wa wilaya ya Mkinga kwani utafanikisha kuajiri takribani watu 8,000. Aidha, Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao. Kuhusu wananchi ambao maeneo yao wamechukuliwa na wawekezaji bila kulipwa fidia, Waziri Mkuu amewahakikishia kuwa wote watalipwa.

“Muwekezaji amenihakikishia kwamba atawalipa wananchi wote wanaodai fidia”. Amesema Majaliwa.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu amesiitiza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli imejipanga kuwatumikia wananchi wote pasipo ubaguzi wa kidini, kisiasa, rangi  na kimapato na kuwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter