Home KILIMO Wakulima washauriwa kuuza kwa bei ya faida

Wakulima washauriwa kuuza kwa bei ya faida

0 comment 64 views

Mtaalamu wa Kilimo Biashara mkoani Mbeya, Robart Mwaluseke amewataka wakulima kuacha mazoea ya kuhifadhi mazao wakisubiri bei ipande ana badala yake amewashauri kuuza kwa bei yoyote wanayoona inawaletea faida. Mwaluseke ametoa wito huo katika mkutano wa wadau wa kilimo wilayani Mbarali na kusema kuwa, tabia ya wakulima kufanya hivyo inapelekea ongezeko la gharama.

Mtaalamu huyo ameeleza kuwa ili wadau wa kilimo waweze kufanya vizuri katika sekta ya kilimo biashara, wanapaswa kuwa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu za gharama zinazotumika wakati wa uzalishaji ili baada ya mavuno, waweze kulinganisha gharama walizotumia na bei iliyopo sokoni.

“Kuna mtu anaweza akauza mazao yake kwa bei kubwa na bado akaingia hasara na mwingine anaweza akauza kwa bei ya kawaida na akapata faida kubwa, hivyo tunawashauri wakulima wabadilike”. Amefafanua Mwaluseke.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Mradi wa Nafaka wa Shirika la USAID, Idd Kindamba  amewashauri wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kuanzisha utaratibu wa kupata pembejeo za kilimo ili kuongeza ufanisi katika kilimo chao. Mbali na hayo, Kindamba ameeleza kuwa, kinachopelekea wakulima wengi kupata hasara ni kutokuwa na umoja na kuwashauri wakulima kuwa kitu kimoja ili kusimamia kilimo chao

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter