Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Dkt. Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa

Rais Dkt. Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa

0 comment 206 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito na kuwakaribisha wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuangalia fursa kuwekeza Zanzibar katika maeneo mbalimbali.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji kati ya Ufaransa na Zanzibar kutoka kwa ujumbe wa wafanyabiashara wa makampuni 20 ya Ufaransa katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyatty Zanzibar Mei 29, 2024.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi amesema sera kuu ya uchumi wa Zanzibar ni uchumi wa buluu hivyo amewakaribisha kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya utalii wa fukwe, urithi, michezo na mikutano, sekta ya bandari.

Nyingine ni sekta za mafuta na gesi, bandari ikiwemo ya makontena , uvuvi pamoja na meli za usafirishaji wa mizigo na abiria.

Pia amebainisha fursa za miradi ya miundombinu ikiwemo barabara, viwanja vya ndege , sekta ya nishati na maji, pamoja na kilimo cha viungo.

Rais Dkt. Mwinyi amewahikikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mazingira mazuri kikamilifu ya kufanya biashara na uwekezaji.

Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui , Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini na Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la MEDEF kutoka Ufaransa, Gerald Wolf.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri na sekta binafsi wameshiriki mkutano huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter