Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali yafuta tozo kuwavuta wawekezaji

Serikali yafuta tozo kuwavuta wawekezaji

0 comment 144 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, serikali imefuta baadhi ya tozo na ada zisizoondoa wajibu wa muajiri kulinda afya za wafanyakazi ili kuunga mkono azma ya kufikia uchumi wa viwanda.

Mhagama ameeleza kuwa mabadiliko mbalimbali yamefanywa katika Mamlaka ya usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) ili kuchangia azma ya serikali kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wawekezaji. Mhagama amefafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuboresha mazingira ya biashara pamoja na kushusha gharama za uendeshaji kwa wawekezaji na waajiri.

“Tumefuta ada mbalimbali ikiwemo ada ya fomu ya usajili ambayo ilikuwa Sh. 2000 kwa lengo la kupunguza gharama, tumefuta ada ya usajili wa maeneo ya kazi kwa kuzingatia ukubwa wa eneo ambayo ilikuwa ikitozwa kwa kiasi cha Sh. 50,000 hadi 1,800,000 kulingana na eneo hivyo usajili kwa sasa ni bure”. Amesema Waziri huyo.

Aidha, Mhagama ametangaza kuwa serikali imefuta leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya usalama na afya mahali pa kazi ya Sh. 200,000 kwa mwaka ambapo amebainisha kuwa leseni hiyo itatolewa bure kwa sasa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter