Home BIASHARA Wafanyabiashara Tanzanite watoa mamilioni

Wafanyabiashara Tanzanite watoa mamilioni

0 comment 122 views

Waziri wa Madini, Doto Biteko, amesema wafanyabiashara wa Tanzanite, Simanjiro mkoani Manyara wamelipa kodi ya Shilingi bilioni 1.4 kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia Disemba mwaka jana. Biteko amesema hayo wakati anamkabidhi Mkandarasi Suma JKT sehemu ya kujenga kwa ajili ya wanunuzi wadogo, wakubwa pamoja na madalali, pamoja na kufunga kamera za kielektroniki kuzunguka ukuta wa mgodi huo.

Waziri huyo amesema wafanyabiashara hao wa madini wameanza kuelewa umuhimu wa ulipaji kodi na kufuata kanuni za biashara, ndio maana serikali imeweza kukusanya kodi kiasi hiko jambo ambalo halijatokea kwa muda mrefu.

“Hadi kufikia Disemba mwaka jana wafanyabiashara wa Tanzanite Mererani wamelipa kodi zaidi ya Shilingi bilioni 1.4. Pesa hiyo ilikuwa haijawahi kulipwa kwa kipindi cha miaka mingi sana sasa wafanyabiashara wa Tanzanite wameanza kuwa waelewa wa kulipa kodi ya serikali”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kulipa kodi na kufuata Sheria kwani kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa Sheria. Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Justin Nyari, amesema chama hicho kinashirikiana ipasavyo na serikali kwa kuhakikisha kila mfanyabiashara analipa kodi ili kuongeza pato la taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter