Home BIASHARA Wafanyabiashara wanaochezea vipimo waonywa

Wafanyabiashara wanaochezea vipimo waonywa

0 comment 83 views

Ofisa Elimu, Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) Paulus Oluochi ametoa onyo kwa wafanyabiashara wenye tabia ya kuchezea vipimo na kusisitiza kuwa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa sheria. Katika maelezo yake, Ofisa huyo ameeleza kuwa, Sheria ya vipimo sura namba 340 na mapitio yake ya mwaka 2002 inasema kwa kosa la kwanza ya kuchezea vipimo faini sio chini ya Sh. 300,000 na zaidi ya Sh. 50 milioni au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

“Kosa la pili au kujirudia faini yake haipungui Sh. 500,000 na isiyozidi Sh. 100 milioni au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja”. Amedai Oluochi.

Mbali na hayo,Ofisa huyo kutoka WMA pia amewashauri wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo ili kuepuka usumbufu wanapovinja sheria. Aidha, Oluocho ametoa wito kwa wajasiriamali kuzingatia vipimo katika bidhaa zao kama ambayo Sheria inaelekeza ili kushindana kikamikifu sokoni na kuwataka wajasiriamali kuacha tabia ya kukadiria ujazo wa bidhaa zao katika vifungashio.

“Unakuta bidhaa imeandikwa kilogramu mbili lakini kumbe imekadiriwa tu na kiasi hicho hakijafika katika ujazo huo, hali hii inachangia bidhaa hizo kushindwa kushindana na zile za wafanyabiashara wakubwa”. Amesema Oluochi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter