Home FEDHABIMA Maelfu ya Watanzania wajitokeza matibabu ya bure

Maelfu ya Watanzania wajitokeza matibabu ya bure

0 comment 86 views

Maelfu ya Watanzania wamejitokeza kupata huduma za matibabu bure zinazotolewa na Melivita ya matibabu iitwayo ‘Peace Ark’ ya Jeshi la Ukombozi la watu wa China.

Pesatu imeshuhudia wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za afya kwenye meli hiyo iliyo tia nanga katika bandari ya Dar es Salaam Julai 16, 2024.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea meli hiyo Julai 21, 2024 na kukagua utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi pamoja na kujionea aina ya huduma zinazotolewa na timu ya madaktari bingwa na bobezi wa meli ya Jeshi la Ukombozi (PLA) la Jamhuri ya Watu wa China.

Amesema, Meli hii ilipanga kuona na kutoa huduma za kiafya kwa wagonjwa 600 lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa wananchi, wataalamu hawa wanaona wagonjwa zaidi ya elfu 1,000 kwa siku.” Amesema Waziri Ummy

“Huduma zinazotolewa na wataalamu hawa wa kichina wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni pamoja na uchunguzi, matibabu ya aina zote za magonjwa ya nje, magonjwa ya upasuaji na upasuaji wa kutumia roboti, magonjwa ya mifupa, uzazi na magonjwa ya kinamama, kutibu kwa kutumia tiba asili, magonjwa ya njia ya chakula pamoja na huduma za wagonjwa mahututi (ICU).

Aidha, Waziri Ummy amesema meli hiyo ni hospital inayotembea ikiwa na vipimo vyote vinavyohitajika ikiwemo CT-Scan, Ultra Sound pamoja na vyumba nane vya upasua na madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya ndani.

“Hii ni Hospitali inayotembea kwakweli ina vitu vyote muhimu vinavyohitajika lakini pia kuna vyumba nane vya upasuaji, wana madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani, magonjwa ya moyo, meno na huduma zote muhimu,” Amesema Waziri Ummy.

“Kwakweli nimefurahi kuonana na mama aliyepata mtoto kwa kujifungua salama kwenye meli hii, hii inaonesha kuwa mahusiano ya nchi hizi mbili yamegusa maisha ya watu na mtoto huyu amepewa jina la ‘Peace of Ark’,” amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter