Home FEDHA Dk. Pima: Hatujawahi kukusanya mapato chini ya 85%

Dk. Pima: Hatujawahi kukusanya mapato chini ya 85%

0 comment 109 views

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua, Dk. John Pima amesema halmashauri hiyo hukusanya mapato ya ndani yasiyopungua asilimia 85 ya malengo yake. Dk. Pima amesema hayo wakati wa kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa rasmi kwa halmashauri hiyo ambapo amesema kuwa, halmashauri hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa ujumla katika makusanyo ya ndani. Dk. Pima ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwake, wameweza kukusanya mapato ya ndani kiwango cha asilimia 85 kikiwa ni cha chini kabisa huku asilimia 130 ikiwa ndio kiwango cha juu kwa mwaka wa fedha uliopita, na kupelekea halmashauri hiyo kuwa ya nne kitaifa katika ukusanyaji wa mapato.

 

“Kazi kubwa imefanyika katika kipindi hiki tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana, ushirikiano huu, watendaji mzidi kuchapa kazi na kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa”. Ameeleza Dk. Pima.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter