Fedha ni jambo linalomhusu kila binadamu kwa namna moja au nyingine. Ni moja ya vitu vinavyoamsha hisia za binadamu wote. Fedha imepewa nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu ya kila siku kutokana na ukweli kwamba yenyewe ndio inaendesha maisha yetu. Bila fedha hakuna huduma wala mahitaji muhimu.
Watu wengi wamekuwa wakipata changamoto kubwa kwenye kutunza akiba. Kundi kubwa la watu hasa vijana wamekuwa na matumizi makubwa na asilimia kubwa hawana akiba ya aina yoyote. Kuwa na akiba kuna umuhimu mkubwa na jamii inapaswa kuweka mazoea ya kutunza fedha hata kama kile unachoingiza ni kidogo. Zifuatazo ni mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili kutunza fedha na kuweka akiba:
- Kuwa na bajeti
- Kuwa na nidhamu ya fedha
- Kuwa na rekodi ya matumizi
- Epuka madeni
- Jiwekee malengo na jitahidi kuyafikia
- Jipunguzie kipato kwa asilimia
- Kuwa makini na matumizi yako
- Wekeza kidogo kidogo
Maendeleo ya wananchi hupelekea maendeleo ya taifa kwa ujumla. Kutunza fedha ni kujihakikishia usalama wa maisha ya baadae. Kuweka akiba ni jambo la msingi, tuanze kufanya hivyo sasa.