Home FEDHAMIKOPO Mkopo wa mabilioni wanukia

Mkopo wa mabilioni wanukia

0 comment 78 views

Benki ya Credit Suisse ya Uingereza imeonyesha dhamira ya kutoa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Sh. 455 bilioni (Dola Milioni 200 za Marekani) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na umeme na miundombinu ya reli.

Katika mkutano uliofanyika kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango na ujumbe wa benki hiyo uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Lawrence Fletcher, Dk. Mpango amebainisha kuwa pande zote mbili tayari zimefikia hatua kadhaa katika kufanikisha upatikanaji wa mkopo huo.

Dk. Mpango ametaja baadhi ya miradi itakayopewa kipaumbele kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa (SGR), ununuzi wa ndege mpya ili kufufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na miradi mikubwa ya umeme ambayo itachochea maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Credit Suisse Lawrence Fletcher amesema benki hiyo inaangalia uwezekano ya kufadhili miradi yenye kipaumbele kwa serikali ili kuisadia kutimiza lengo lake la kufikia uchumi unaotegemea viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter