Home FEDHAMIKOPO Mkopo wafurahisha wakulima wa kahawa

Mkopo wafurahisha wakulima wa kahawa

0 comment 121 views

Mkopo wa Sh. 27.2 bilioni uliotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa lengo la kuendeleza kilimo cha kahawa mkoani Kagera umeonekana kuzaa matunda baada ya uzalishaji wa zao hilo kuongezeka na kufikia kilo 33 milioni ikilinganishwa na kilo 5 za msimu uliopita.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani humo Robart Kashambo amesema mkopo huo umewapa imani kubwa wadau wa kahawa na kuongeza kuwa, kupitia TADB wakulima wengi wamekombolewa kupitia malipo ya awali ya wakulima yanayofanywa kupitia vyama vya ushirika ambavyo ni pamoja na KDCU, KCU na Chama cha wakulima wilaya ya Ngara.

“Mabadiliko yaliyofanywa na serikali msimu wa mwaka 2018/2019 tayari takribani kilo milioni 33 zimeshakusanywa kutokana na mkopo uliotolewa na TADB. Kwa sasa tuna zaidi ya Sh. 25 bilioni zimeingia kutoka benki ya kilimo na hii imepunguza makali kwa wakulima kupata fedha kwa wakati”. Amesema Kashambo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Japhet Justine amesema benki hiyo imedhamiria kutekeleza kwa vitendo malengo ya serikali kuwezesha wakulima kupitia vyama vya msingi kama alivyoagiza Waziri Mkuu.

“Kwa muda mrefu vyama hivi vilihitaji kuwezeshwa kimtaji kutokana na kushindwa kupata mikopo kupitia mabenki ya kibiashara sababu ya madeni ya muda mrefu. Mikopo hii imeweza kuvijengea vyama hivi uwezo”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter