Home FEDHA Passport zaingiza mabilioni serikalini

Passport zaingiza mabilioni serikalini

0 comment 201 views

Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Anna Makakala amesema katika kipindi cha Januari mpaka Novemba 25 mwaka huu, Idara hiyo imefanikiwa kukusanya Sh. 7.8 bilioni kutokana na utoaji wa huduma ya hati za kusafiria pekee. Makakala ametoa takwimu hizo wakati akizindua mfumo wa kielektroniki wa Visa na Vibali vya ukazi na kueleza kuwa, mpaka sasa Idara ya Uhamiaji imefanikiwa kutoa hati 55,177 za kusafiria kwa watanzania.

“Tumefanikiwa kutoa pasipoti mpya za kielektroniki (e-Passport) 55,177 kwa raia wa Tanzania tangu Januari 31 hadi kufikia Novemba 25, mwaka huu. Aidha, Sh. 7,887,710,000 zimekusanywa kutokana na huduma ya pasipoti pekee”. Amesema Kamishna Jenerali huyo.

Katika maelezo yake, Makakala amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika hazi hizo mpya za kusafiria ambayo ni awamu ya kwanza ya mradi wa Uhamiaji Mtandao ni pamoja na hati hizo kupatikana kwa urahisi na kwa muda mchache. Kamishna huyo amesema tayari mikoa takribani 25 hapa nchini imepatiwa huduma hiyo, huku mchakati ukiendelea katika mikoa minne iliyobaki bara pamoja na Zanzibar.

Kamishna Jenerali huyo amedai kuwa Idara ya Uhamiaji imekusanya Sh. 161,669,471,498,59 ambayo ni sawa na 89.42 ya malengo huku wakitarajia kukusanya zaidi mwaka wa fedha 2018/2019 kutokana na mifumo ya kisasa iliyozinduliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter