Home Elimu Wanahabari za michezo kunolewa kwa ajili ya AFCON

Wanahabari za michezo kunolewa kwa ajili ya AFCON

0 comment 146 views

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye amesema Serikali kupitia Wizara anayoiongoza na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, itawezesha mafunzo ya ndani na nje ya nchi kwa waandishi wa habari za michezo kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Akifungua TASWA Media Day Bonanza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa katika viwanja vya Msasani Beach Club, Dar es Salaam, Februari 10, 2024, Waziri Nape amesema, “Serikali kupitia Wizara ya Habari na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo tutandaa mafunzo pamoja na safari za nje ya nchi kwa waandishi wa habari za michezo ili kujiandaa vizuri katika kutoa habari za mashindano ya AFCON 2027.

Wanahabari ni watu muhimu katika kutangaza nchi yetu. Tunapenda kuwapa mafunzo na vifaa ili waweze kutangaza mashindano hayo kwa ufanisi.”

Aidha, Waziri Nape amewataka wanahabari kuepuka kuandika habari zinazowavunja moyo wa wanamichezo wa Tanzania, akisisitiza kuwa michezo ni mchanganyiko wa mafanikio na changamoto, hivyo ni muhimu kutoa msaada na uungwaji mkono kwa wanamichezo wetu.

“Tusiandike habari zinazowavunja moyo wanamichezo wetu,” amesisitiza.

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter