Home FEDHA Serikali yatoa Bilioni 83/- kununua korosho

Serikali yatoa Bilioni 83/- kununua korosho

0 comment 99 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema hadi kufikia Desemba 08 mwaka huu, serikali imefanikiwa kuwalipa wakulima 82,835 kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya Sh. 83 bilioni imelipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ambapo katika mkoa wa Mtwara wakulima 50,835 wamelipwa, mkoa wa Lindi wakulima 22,131 na mkoa wa Ruvuma wakulima 9,445.

Waziri Hasunga amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro. Hasunga amesema hadi sasa jumla ya vyama 328 kati ya vyama 504 vimefanyiwa uhakiki katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya vyama 319 vimekwishalipwa tayari.

Aidha, Waziri huyo ametumia nafasi hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaopotoshwa na madai kuwa bado wakulima hawajalipwa kiasi chochote cha fedha na serikali, huku akisisitiza kuwa wakulima wanalipwa kwa njia ya benki an kuataka wananchi kuwa na utamaduni wa kwenda benki.

Hasunga amesisitiza kuwa serikali inalenga kuwanufaisha wakulima wa korosho, na kueleza kuwa tayari ametoa maelekezo kwa watendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania kusajili wakulima wote wa korosho ili watambulike kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wananufaika hivyo korosho zote zitabanguliwa hapa nchini.

“Tulipoona soko la korosho linayumba huku lengo la serikali likiwa ni kutaka kuona wakulima wananufaika, tuliamua kuingilia kati na kuanza kununua korosho zote na kwa kwenda mbele zaidi tumeamua kubangua korosho zote hapa hapa nchini”. Amesema Waziri huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter