Home KILIMO Naibu Waziri atoa siku tatu kwa TCB

Naibu Waziri atoa siku tatu kwa TCB

0 comment 79 views

Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa, ametoa muda wa siku tatu kwa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhakikisha kila mkulima wa pamba mkoani Simiyu anapata mbegu za kutosha. Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo wilayani Bariadi baada ya kukutana wakulima wa zao hilo waliolalamika kutopatiwa mbegu za kutosha kutoka TCB japokuwa tayari msimu wa kilimo umeanza Wakulima hao wamemueleza Naibu huyo kuwa, wanapatiwa mbegu chache kulingana na mahitaji halisi.

“Tatizo letu kwa sasa ni mbegu, hazipatikani kwa wakati, tunapewa chache, mimi nimepata kilo 15 lakini mahitaji ni 50, mwaka huu tumeangaika, tunaomba mbegu”. Ameeleza mmoja wa wakulima hao

Mbali na hayo, Bashungwa amemuagiza Meneja wa TCB Kanda ya Ziwa, Jones Bwahama, kubaki mkoani Simiyu baada ya ziara yake ya siku mbili ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu za pamba kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter