Zaidi ya eka 30,000 za mahindi mkoani Pwani zimeharibiwa na panya ambao wamekuwa wakivamia mashamba na kula mazao hayo. Baadhi ya kata zilizokumbwa na janga hilo ni pamoja na Bwewe, Lugoba, Kibundu na Mandela. Akizungumzia kuhusu uharibifu huo, Diwani wa kata ya Kibindu Ramadhani Mkufya amesema uharibifu huo umeanza tangu msimu wa vuli na unazidi kuongezeka na hivyo kuleta hasara kwa wakulima. Mbali na kula mahindi, panya hao pia wanakula mpunga na kufukua viazi. Baraza la madiwani la Chalinze limetoa agizo kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Edes Lukoa kuwasiliana na mamlaka husika ili suluhisho la haraka lipatikane na uharibifu unaoendelea udhibitiwe.
62