Home FEDHA Taasisi  ya Bill Gates yatoa bilioni 777 Tanzania

Taasisi  ya Bill Gates yatoa bilioni 777 Tanzania

0 comment 108 views

 

Na Mwandishi wetu

Tajiri namba mbili duniani Bill Gates ambaye kwa sasa yupo nchini Tanzania amesema kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates imetenga dola za kimarekani milioni 350 ambazo ni sawa na takribani Sh 777 bilioni ili kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini.

Gates alitoa kauli hiyo Ikulu Dar es salaam alipokuwa na mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli. Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi Dk. Charles Tizeba na Waziri wa Afya, Jamii na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.

Fedha hizo zitaelekezwa zaidi katika sekta ya afya ili kupambana na matatizo ya vifo vya uzazi, malaria, lishe bora na utapiamlo. Sekta nyingine zitakazonufaika ni pamoja na ya kilimo ambayo inategemewa kuboresha uzalishaji wa mazao, upatikanaji wa mbegu bora na kuimarisha shughuli za ufugaji. Kwa kufanya hivyo, upatikanaji wa chakula nchini utakuwa ni wa uhakika.

Rais amemshukuru Bill Gates kwa msaada mkubwa taasisi yake uliyojitolea na kuahidi kuwa zitatumika katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini kote.

Wakati huo huo pia, serikali ya marekani kupitia Balozi wake nchini Dk.. Inmi Patterson itatoa Sh 499 bilioni mwaka ujao kusaidia miradi ya afya, elimu, lishe na utawala bora. Balozi huyo amesema kuwa Marekani ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na Tanzania hivyo itasaidia miradi ya maendeleo nchini hapa kutekelezwa.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter