Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Jinsi ya kutambua bidhaa feki

Jinsi ya kutambua bidhaa feki

0 comment 223 views

Imekuwa ni kawaida kuona bidhaa mbalimbali zikitengenezwa na kuuzwa kwa bei sawa na bure. Mara nyingi bidhaa zenye ubora na kiwango cha juu huwa zinauzwa gharama kwa sababu wazalishaji huwa wanatumia muda na fedha nyingi kuhakikisha bidhaa zao zina ubora wa hali ya juu na zipo tofauti na bidhaa nyingine za kawaida.

Licha ya hivyo, soko la kutengeneza kopi linaendelea kukua na kila siku watu wananunua bidhaa za bandia kila siku.

Kutokana na hilo, unawezaje kugundua bidhaa feki?

Ifahamike kuwa si kila bidhaa feki huuzwa bei ndogo, lakini unatakiwa kuwa makini na mkataba unaotolewa na muuzaji. Wafanyabiashara wa bidhaa feki hupendelea kutoa mkataba ambao unaweza kumfanya mteja atafakari mara mbili kuhusu bidhaa husika.

Siku zote bidhaa halisi huwa na mfumo madhubuti katika upande wa vifungashio na muonekano wake kutokana na kwamba, fedha nyingi hutumika katika manunuzi ya vifaa kwa ajili ya kufanya hivyo. Bidhaa feki hutumia vifaa na malighafi za bei rahisi kukamilisha muonekano. Katika bidhaa feki ni rahisi kuona ngozi bandia, glasi ya bei nafuu, kitambaa cha bei rahisi nk vimetumika kutengeneza bidhaa, jambo ambalo linaweza kupelekea muundo wake kubadilika. Kwa kupitia ubora wa malighafi zilizotumika ni rahisi kujua kama bidhaa ni feki au halali.

Makosa katika herufi zilizopo katika bidhaa kwa mfano jina la bidhaa huashiria kuwa bidhaa hiyo ni feki. Ni kawaida kuona bidhaa feki zinakosa baadhi ya herufi au hubadilisha sehemu kubwa ya jina la bidhaa husika. Kwa mfano badala ya kusema “Louis Vuitton” kwenye bidhaa feki utakuta imeandikwa “Vitton”. Hii inaonyesha moja kwa moja kuwa, bidhaa hiyo sio halali.

Kama ilivyo kwenye makosa ya herufi, hata nembo za bidhaa hutofautiana katika bidhaa feki.  Ili kuweza kutambua tofauti unaweza kulinganisha nembo ya bidhaa unayofikiria kuwa ni feki pamoja na nembo halali. Kwa mfano ili kujua Samsung feki kupitia nembo ni rahisi kwa sababu nembo yake halali Samsung sio pana, na maneno yake yameandikwa katika maandishi madogo, lakini Samsung feki huwa na nembo kubwa kidogo huku maandishi yake yakiwa mapana.

Bidhaa feki ni biashara kwa watu wengine lakini soko hili linaendelea kuwaumiza wauzaji wa bidhaa halali na kusababisha kupoteza wateja ambao hufurahia vitu vya bei rahisi, pia jina la biashara linaweza kuharibiwa. Taasisi husika zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali kuelimisha wananchi kuhusu bidhaa bandia pamoja na kuteketeza bidhaa hizo kabla hazijafika sokoni na kuleta athari zaidi. Elimu zaidi inapaswa kutolewa kwa wananchi ili biashara hii ifike kikomo.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter