Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Kibegi, jezi za Simba zilizopandishwa Ml. Kilimanjaro zaleta Sh 29m

Kibegi, jezi za Simba zilizopandishwa Ml. Kilimanjaro zaleta Sh 29m

0 comment 112 views

Klabu ya Simba imefanya mnada wa kibegi na jezi zilizopandishwa Mlima Kilimanjaro kwa Sh29 milioni.

Jezi hizo za msimu wa mashindano 2023/24, zilizinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 21, 2023.

Jezi hizo za aina tatu ambazo zimepigwa mnada ni zenye majina ya viongozi, Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Pia, kuna ya Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Taarifa ya klabu ya Simba inaeleza kuwa katika mnada huo jezi ya Rais Dk. Samia imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 huku ile ya Rais Dk Mwinyi imeuzwa kwa Sh 5,000,000.

Jezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imenunuliwa kwa Sh. 4,000,000 na ya Makamu wa Rais Dk. Mpango imeuzwa Sh. milioni 3.

Katika manada huo, milioni 2,500,000 zilitolewa kununua jezi ya Spika wa Bunge Dk. Tulia huku jezi ya Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji ikinunuliwa kwa Sh. 2,000,000.

“Kibegi kilichokuwa na jezi zetu na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kimeuzwa kwa Sh. 2,500,000,” imesema taarifa hiyo.

Fedha zilizopatikana katika mnada huo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa ya Zanzibar (Mnazi Mmoja).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter