Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Vyakula vya mifugo ikiwemo samaki vyaondolewa VAT

Vyakula vya mifugo ikiwemo samaki vyaondolewa VAT

0 comment 55 views

Vyakula vya mifugo vinavyoingizwa nchini ikiwemo vyakula vya Samaki vinavyotambulika kwa HS Code 23.09 chini ya utaratibu wa utozaji ushuru wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vimepewa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchema wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Jacqueline Ngonyani Msongozi, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupunguza kodi ya uingizaji wa vyakula vya samaki nchini.

‘’Vifaa vinavyoagizwa kutoka nje na watu wanaojihusisha na ufugaji wa samaki na kilimo ambavyo Kamishna ameridhika kuwa ni kwa matumizi katika sekta ya ufugaji wa samaki vimeondolewa Ushuru wa Forodha kwa mujibu wa Kifungu cha 15(a) cha Sehemu B ya Jedwali la Tano ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema Waziri Dkt. Nchemba.

Dkt. Nchemba amefafanua kuwa Serikali inaendela kuongea na sekta ili kuona maeneo ambayo yanastahili kupata ruzuku na tayari baadhi ya maeneo Serikali inatoa ruzuku na itaendelea kutoa ruzuku katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.

Ameongeza kuwa Serikali inaweka vivutio kwenye uzalishaji wa bidhaa ili kujitosheleza ndani ya nchi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kuwa itaangalia maeneo ya maboresho katika bajeti ijayo kufanikisha kuongeza uzalishaji wa ndani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter