Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Kimbilieni kuwezesha waanzisha miradi: Waziri wa Fedha

Kimbilieni kuwezesha waanzisha miradi: Waziri wa Fedha

0 comment 115 views

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za serikali kuwezesha watu wanaoanzisha shughuli za uzalishaji nchini.

Mwigulu amesema hayo katika Kongamano la Kodi Kitaifa lililofanyika jijini Dar es Salaam na kukutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya kodi kujadili namna ya kuboresha Sera za Kodi, kuchochea ukuaji wa uchumi, biashara na uwekezaji nchini.

“Mtu yeyote anaetaka kuanzisha shughuli za uzalishaji watendaji wa serikali wanapaswa kumkimbilia kumwezesha, taasisi za serikali zinatakiwa kupishana mlangoni kuangalia anakwama wapi wamsaidie, wamkwamue,” amesisitiza Mwigulu.

Amesema “tulipotoka nyuma kule kuanzia uhuru kuja huku ambapo serikali alikuwa anafanya kila kitu, watendaji wote huwa wanakimbilia kumdhibiti, watapishana kwenda kumdhibiti, funga, na kuangalia amekosea wapi ili asiendelee.”

Akizungumzia swala la kodi amesema kama makusanyo hayaendelei hakuna namna tunaweza tukapata huduma bora.

“Hivi kunavyokuwa na ongezeko la watu ni lazma makusanyo tuyaongeze kwa uwiano wowote ule, tunahitaji kwa ajili ya mambo ya huduma za afya, elimu, kilimo, miundombinu, usalama na shughuli nyingine, ili tuweze kutimiza haya ni lazma kila mtu aone ni wajibu wake,” ameeleza Waziri Mwigulu.

Amesema takwimu za sensa ya mwaka jana inaonyesha kuwa kuna takribani ya Watanzania milioni 62, ambapo kati yao walipa kodi ni milioni tatu tuu.

“Tuna nguvu kazi kubwa ambayo ingekuwa kazini ingeongeza nguvu ya uchumi kwa kuwa sehemu ya walipa kodi,” amesema Waziri Mwigulu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter