Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Ngorongoro live Dubai

Ngorongoro live Dubai

0 comment 110 views

Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaonekana mubashara (live) kwenye maonesho ya utalii ya Exp2020 Dubai.

Waziri wa Maliasili na Utallii, Dkt. Damas Ndumbaro amepongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa namna inavyotangaza vivutio vya Utalii kwa njia kidigitali kupitia Ngorongoro Live  Streaming  (Matangazo mubashara kutoka Ngorongoro).

Amesema hali hiyo ya Ngorongoro Streaming Live kwenye maonesho hayo inakomesha upotoshaji uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watu wa nchi jirani juu ya vivutio vizuri vya Utalii vilivyopo Tanzania na kusema kuwa vipo nchini mwao.

“Tayari kama nchi tumekuja na njia ya kutangaza vivutio vya utalii kwa njia ya Kiditaji kupitia NgoroNgoro Live  Streaming na imeanza kuonesha matunda ya wazi katika maonesho haya,” Amesema Waziri Dkt. Ndumbaro.

“Tumekuwa tukirusha matukio mbashara kutoka katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, hii imelifanya banda la Tanzania kuwavutia maelfu ya watu kuja kujionea maajabu yaliyopo Tanzania”.

Tunachotaka kwa sasa ni kuhakikisha kuwa Tanzania inashiriki kikamailifu katika maonesho makubwa ya kibiashara huku msisitizo mkubwa kama nchi ni kunadi utajiri wa vivutio vya utalii tulivyonavyo ili kuuondoa ule upotoshwaji wa majirani zetu” amesema Dkt.Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Watanzania popote walipo kutumia fursa ya kunadi vivutio vya utalii walivyonavyo kwani kufanya hivyo ni ishara ya uzalendo kwa nchi yao.

Katika maonesho hayo, kesho Februari 26, 2022 ni Siku ya Tanzania ambapo Rais Samia Suluhu atakuwa mgeni rasmi kwenye Maonyesho hayo na ataeleza kwa undani fursa zilizopo nchini na kuitangazia Dunia kuja nchini kuwekeza.

Miongoni mwa taasisi za Tanzania za Wizara ya Maliasili na Utalii  zinazoshiriki maonesho hayo ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyanapori Tanzania (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Huduma za Misitu Tazania (TFS).

Maonesho hayo ya kimataifa yaliyoanza  Oktoba Mosi mwaka 2021 yanaendelea hadi Machi 31 mwaka huu na yanashirikisha zaidi ya nchi 192.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter