Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Rais Samia ataka wateule wake kujiongeza

Rais Samia ataka wateule wake kujiongeza

0 comment 73 views

“Tumieni taaluma zenu, panapofaa tumia common sense (akili yako), jiongezee” ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wateule wapya wakiwemo Mawaziri na viongozi mbalimbali.

Rais Samia amesema hayo Agosti 15, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha voiongozi wateule.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani amesema mabadiliko anayoyafanya katika baraza la Mawaziri na viongozi wengine mbalimbali ni ya kawaida na katika kuongeza ufanisi.

“Mabadiliko haya ni ya kawaida na katika kuongeza ufanisi kwenye maeneo yetu, na Makamu wa Rais amesema vizuri tunachotegemea ni ufanisi, kwenda kuongeza ufanisi kwenye maeneo yenu.

Kama mnavyoelewa nina safari sasa hivi ya kwenda kwenye vikao vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na kwa maana hiyo sitaongea na ninyi leo, lakini nitawaita kwa sekta zenu siku moja moja tuje tuzungumze kwa undani zaidi,” amesema Rais Samia.

Amewataka viongozi hao kutenda kazi kwa utaalamu sambamba na kujiongeza kwa kutumia akili zao pale wanapoona inaweza kutumika vizuri.

“Mjiongeze, tufanye kazi tuwatumikie wananchi,” amehitimisha Rais Samia.

Agosti 14, 2024, Rais Samia alifanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, Mwanasheria Mkuu, uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Wilaya.

Wengine ni Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na wakuu wa taasisi mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter