Home VIWANDAMIUNDOMBINU Precision Air yazindua safari za Kahama leo

Precision Air yazindua safari za Kahama leo

0 comment 53 views
Na Mwandishi wetu

Shirika la ndege la Precision leo hii limezindua safari mpya ya Kahama ambapo majira ya saa 12 alfajiri, ndege aina ya ATR42-500 ya shirika hilo iliondoka kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es salaam na kutua Kahama saa mbili asubuhi kisha kurejea jijini Dar es salaam kupitia mkoa wa Tabora.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack ambaye alikuwa miongoni mwa abiria walioondoka katika safari hiyo amesema safari hiyo imekuja baada ya jitihada za muda mrefu zilizofanywa na uongozi wa mkoa na wilaya ya Kahama kuzungumza na shirika hilo.

Amesema kuwepo kwa safari hiyo kutawasaidia wananchi katika mkoa wa Shinyanga kufanya safari kwa urahisi zaidi kwani hapo awali iliwalazimu wakazi wa Bukombe kusafiri hadi Mwanza ili kupata usafiri wa ndege.

Naye Meneja Mratibu wa bidhaa wa Precision Air Hillary Mremi amesema safari hiyo imeanzishwa kama muendelezo wa mipango ya shirika hilo kuunganisha Tanzania. Ameongeza kuwa Kahama ni mji wenye fursa nyingi za kibiashara hivyo ni lazima kuwe na safari za ndege huku akidai soko la shirika hilo katika usafiri wa anga litaongezeka kwani mji huo bado haujafikiwa na huduma za usafiri wa ndege.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter