Na Mwandishi wetu
Hospitali ya Afya ya Akili iliyopo Korogwe mkoani Tanga imekuwa inawasaidia baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya wanaopelekwa katika hospitali hiyo kwa kuwafundisha namna ya kutengeneza samani kama viti vya nyumbani na hotelini pamoja na kapeti ili kuwaandaa kuwa wajasiriamali pindi watakapomaliza matibabu yao.
Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo, Amina Ramadhani amesema baada ya kupokea wagonjwa hawa, wanakaa nao kwa kipindi fulani na wakionyesha maendeleo mazuri kiafya, wanapatiwa elimu ya ufundi wa kutengeneza samani ambayo wengi wamekuwa wakifanya vizuri. Hii inawasaidia kutumia muda wao vizuri badala ya kukaa bila kazi.
Fursa hii wanayopewa wagonjwa inawasaidia kuondokana na utegemezi mara baada ya kupona kwani wanakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kujiingizia kipato kutokana na bidhaa wanazotengeneza ambazo soko lake kubwa ni Wilaya ya Bagamoyo