Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI TEHAMA: Fursa mpya ya kukuza uchumi

TEHAMA: Fursa mpya ya kukuza uchumi

0 comment 96 views

Ukuaji wa teknolojia umekuwa wa kasi hapa nchini. Kumekuwa na fursa nyingi za biashara kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia. Watu wengi zaidi wamekuwa wakihamia katika sekta hii ili kujiingizia kipato kwa kuajiriwa, kujiajiri au kuwekeza. Teknolojia imekuwa tumaini jipya kwa wengi hivi sasa. Mbali na kutoa fursa mbalimbali za biashara, ukuaji wa teknolojia pia umeboresha shughuli za viwandani.kama unafikiria kuwekeza katika masuala ya teknolojia, unaweza kufanya hivyo kwa namna zifuatazo.

Kupitia teknolojia, kuna fursa nzuri ya kuanzisha biashara katika maeneo ya vijijini ambayo bado hayajafikiwa na umeme. Umeme jua umekuwa mkombozi wa wengi. Teknolojia hii hutumika kwa wingi kama namna moja wapo ya kujiajiri na kujiingizia kipato. Matumizi mbalimbali ya umeme yanaweza kuendelea kupitia teknolojia hiyo hivyo mjasiriamali anaweza kutumia vifaa hivyo na kuanzisha biashara ya vinywaji baridi, kuchaji simu, mgahawa mdogo na nyingine nyingi zitakazomuwezesha kujiingizia kipato kizuri tu.

Mbali na hayo pia unaweza kuwekeza katika teknolojia kwa kukuza biashara yako mtandaoni. Hapa utahitaji kuwekeza muda zaidi kuliko fedha. Wengi hufanya biashara mitandaoni lakini tofauti inakuja katika ubora wa biashara yako pamoja na namna unavyohudumia wateja wako. Japokuwa mawasiliano yatafanyika kwa asilimia kubwa kupitia mitandao ni vizuri kuhakikisha kuwa unatoa huduma bora zaidi za usafirishaji kwa wateja watakao kuwa mbali na pia tumia muda ako kuwasikiliza wateja na kuwapa huduma bora zaidi.

Unaweza kuwekeza kwenye tovuti na kupata kipato kutokana na matangazo pamoja na taarifa unazoandaa. Wengi wameweza kupata ajira kutokana na kuanzisha tovuti hivyo vya kuwekeza kiasi kidogo katika biashara hii unaweza kufaidika kwani aina hii ya teknolojia inaendelea kukua kwa kasi hivyo soko nalo katika biashara hii linaendelea kukua siku hadi siku.

Uwekezaji huu unazo changamoto zake lakini unaonyesha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Watu wengi wanaendesha maisha yao kwa njia hii na wengi zaidi wamekuwa wakitamani kufanya biashara kwa kutumia mifumo ya teknolojia. Lakini ili uchumi wetu uimarike kupitia sekta hii ni vizuri kutoa elimu za kompyuta mashuleni na kuwazoesha wanafunzi kuelewa teknolojia kuanzia ngazi ya elimu ya msingi, ni vizuri kuwe na upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu ili watu wengi zaidi wapate kufikiwa na pia ni muhimu kwa makampuni na taasisi mbalimbali kuwekeza katika teknolojia ili kuwaonyesha njia wawekezaji wadogo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter