Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali Tanga wabanwa

Wajasiriamali Tanga wabanwa

0 comment 76 views

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amesema mkoa huo utawachukulia hatua kali wajasiriamali watakaoendelea kufanya biashara zao pasipo kuwa na vitambulisho rasmi ambavyo baada ya Januari 21 mwaka huu, vitatolewa kwa malipo ya Sh. 20,000 na kuwataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kusimamia zoezi la kutoa vitambulisho na kuwachukulia hatua watakaokaidi agizo hilo kwa wakati.

Shigella ametoa onyo hilo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Korogwe na kuwaeleza wajasiriamali pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa, baada ya Januari 21 hakuna atakayeruhusiwa kuendesha biashara bila ya kuwa na kitambulisho na Sheria zitachukuliwa dhidi ya atakayebainika kukiuka maagizo hayo.

“Baada ya tarehe 21 mjasiriamali atakayekutwa anafanya biashara huku akiwa hana kitambulisho tutamkamata na kuuza mali zake ili tupate elfu 20,000 yetu kinachobaki anarejeshewa. Ndugu zangu sitarajii yawafike haya lipeni hiyo hela mffanye shughuli zenu kwa uhuru”. Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter