78
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Vodacom imetoa msaada wa kompyuta 30 kwa shule ya msingi Mbwanga mjini Dodoma. Hii ni katika juhudi za kampuni hio kusaidia mpango wa serikali wa kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuhakisha wanafunzi wanapata elimu ya kidijitali kuanzia elimu ya msingi .