Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wasomi washauriwa kuchangamkia kilimo

Wasomi washauriwa kuchangamkia kilimo

0 comment 150 views

Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amewasahuri wahitimu kugeukia sekta ya kilimo na kuangalia uwezekano wa kujiajiri hususani kwenye biashara kupambana na changamoto ya ajira. Beng’i ametoa wito huo wakati akifungua semina kwa wahitimu wa shahada za jinsia na maendeleo kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Tunafahamu zipo changamoto kwenye soko la ajira hasa kwa wasomi kama nyinyi ndio maana tunahimiza utaratibu wa kujiwekea akiba na kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwani mifuko mingi  huwafikia watu kwa njia hii” Ameeleza Beng’i.

Katibu Mkuu huyo amewataka wasomi kujiunga kwenye vikundi wakiwa na wazo la kutekeleza ambalo litawawezesha kuomba fedha katika mifuko mbalimbali inayowasaidia vijana na kuwashauri kutumia vyema fursa zilizopo kwenye mifuko ya uwezeshaji na kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter