Home KILIMO FAO kuwawezesha wakulima

FAO kuwawezesha wakulima

0 comment 118 views

Shirika la Chakula Duniani (FAO) limeahidi kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mpunga ili waweze kuzalisha kwa kiwango bora na kinachoendana na wakati. Hayo yamesemwa na mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini Fredy Kafeero alipowatembelea wakazi wa tarafa ya Pawaga na Idodi katika wilaya ya Iringa vijijini na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mashine za kisasa za kuvunia.

Akizungumzia kuhusu changamoto hizo, Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji Mkombozi, Saleh Mohammed amesema miundombinu ya duni ya kuvunia imekuwa tatizo kubwa, hali inayowalazimu kufyeka na kusababisha mpunga kupotelea shambani. Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Tuungane , Twalib Ubwa ameomba shirika hilo kuwajengea uwanja wa kuanikia mpunga iwapo watapata kwanza mashine ya kuvunia.

Akizungumza kuhusu maombi hayo, Kafeero amedai moja kati ya kazi zao ni kuzichukua changamoto za wakulima na kuzifanyia kazi.

“Wakulima wana changamoto nyingi na tupo hapa kuzitatua. tutahakikisha tunawapatia mashine za kuvunia ili kuokoa upotevu wa mpunga shambani na kuborsha miundombinu skimu zao kwa kutumia umwagiliaji” Amesema mwakilishi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter