Home KILIMO Sheria ya kilimo inakuja-Waziri Hasunga

Sheria ya kilimo inakuja-Waziri Hasunga

0 comment 103 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuna haja ya Sheria ya kilimo kuanzishwa ili itumike kutoa suluhisho kwa changamoto zinazomkabili mkulima na sekta ya kilimo kwa ujumla. Hasunga amesema hayo wakati wa kikao cha siku mbili na watafiti wa kilimo kutoka taasisi mbalimbali zinazoshughulika na kilimo nchini.

“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka Sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya”. Amesema Hasunga.

Katika maelezo yake, Waziri huyo amesema Sheria zinazotumika hivi sasa ni zile za Bodi za mazao mbalimbali, ambazo pia zina changamoto zake. Pamoja na hayo, pia kuna mazao ambayo hayana Bodi rasmi hivyo kiasi kuwatetea wakulima wa mazao hayo ni changamoto.

Ametaja mazao yaliyopo katika utaratibu wa Bodi kuwa ni pamba, kahawa, chai, korosho, pareto na tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara huku mazao ambayo hayana bodi ni yakiwa yale ya chakula ambayo nayo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa taifa.

Naye Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk. Fortunus Kapinga amesema kikao hicho kimekuja wakati ambapo utafiti ulio na tija unahitajika ili kutatua changamoto katika sekta ya kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter