Home KILIMOKILIMO BIASHARA China yatangaza soko

China yatangaza soko

0 comment 105 views

Ubalozi wa Tanzania Beijing, China umetangaza kuwa kampuni moja nchini humo imewasilisha ombi la kununua karanga, ufuta na maharage ya soya kutoka Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana (Desemba 20, 2018) na kusainiwa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo, kampuni hiyo inatarajia kununua bidhaa hizo kwa vigezo.

 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kampuni hiyo inahitaji ufuta tani 3,000 kwa mwezi, karanga tani 2,000 kwa mwezi pamoja na maharage ya soya tani 5,000 kwa mwezi. Chilambo kutoka TanTrade amesema ufuta unaotakiwa ni ule wa ubora wa taifa daraja la pili na kuongeza kuwa hata karanga na maharage ya soya yanayohitajika ni yale yaliyopo katika kiwango hicho cha ubora.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter