Home KILIMOKILIMO BIASHARA Mfumo wa Crop Stocks Dynamic System warahisihsa utoaji taarifa bei za mazao sokoni

Mfumo wa Crop Stocks Dynamic System warahisihsa utoaji taarifa bei za mazao sokoni

0 comment 321 views

Wizara ya Kilimo inaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu utaratibu wa uuzaji na ununuzi wa mazao ya chakula kupitia Mfumo wa Crop Stocks Dynamics System (CSDS) kwa watalaamu wa kilimo katika ngazi ya Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa ili kurahisisha usajili wa ghala za Umma, vituo vya mauzo na ukaguzi wa mazao.

Katika kuendelea kuboresha Mfumo huo Wataalamu kutoka Idara ya Masoko na Usalama wa Chakula (Agricultural Marketing and Food Security Division) wamefanya ukaguzi maalumu (technical backstopping) ya Mfumo huo katika Mikoa ya Singida, Tabora na Geita ili kubaini ubora, changamoto na maeneo ya kuboresha katika matumizi yake.

Kwa upande wa Singida, wataalamu hao wametembelea Masoko ya Namfua na Soko Kuu la Kimataifa la Vitunguu Misuna yaliyopo katika Manispaa ya Singida ili kujionea namna maafisa ugani wanavyochukua takwimu mbalimbali za mwenendo wa bei za mazao na kuziweka kwenye mfumo huo.

Kwa Mkoa ya Tabora, watalaamu hao wametembelea Soko la Kachoma na Soko Kuu la Tabora ambalo ni maalumu kwa ajili ya biashara ya zao la mahindi na kwa upande wa Mkoa wa Geita wametembelea Soko la Nyankumbu lililopo Halmashauri ya Mji wa Geita.

Wakizungumzia kuhusu Mfumo huo, maafisa ugani wamepongeza jitihada za Wizara kwa kuanzisha mfumo huo kwani umerahisisha kazi ya utumaji wa taarifa ukilinganisha na ilivyokuwa awali kwa njia ya simu pia mfumo umerahisisha utoaji wa taarifa za mwenendo wa bei za mazao sokoni kwa wakati.

Baadhi ya changamoto zilizobainika ni uhaba wa vitendea kazi, mtandao, gharama za kuendesha mfumo pamoja na ushirikiano mdogo kutoka kwa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kutoa bei ya kununulia na siyo bei ya kuuzia.

Mikoa mingine iliyofanyiwa ukaguzi hapo awali ni Mikoa ya Tanga, Pwani pamoja na Morogoro kwa lengo la kupata mrejesho wa changamoto na maeneo ya kuboresha katika matumizi ya Mfumo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter