Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tanzania yahakikishiwa soko la chai Algeria

Tanzania yahakikishiwa soko la chai Algeria

0 comment 23 views

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT), Beatrice Banzi amekutana na Balozi wa Algeria hapa nchini Ahmed Djellal kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa ushirikiano wa kibiashara katika tasnia ya chai.

Kikao hicho kilichofanyikia katika ofisi za Ubalozi zilizopo Upanga, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Meneja Masoko wa TBT Suleiman Chilo.

Balozi Djellal aliihakikishia TBT uwepo wa soko kubwa la chai nchini Algeria kutokana na wananchi wake wapatao milioni 47 kuwa na utamaduni wa kunywa chai.

Pia amebainisha kuwa suala la jiografia ya nchi hiyo nayo inasaidia soko la uhakika kwa kuwa Algeria imepakana na Ufaransa, Hispania na Italia ambapo bidhaa nyingi kutoka Nigeria zinaingia kwenye nchini hizo.

Amesema “itakua vyema kama Chai ya Tanzania itapata masoko Algeria kwa kuwa itakuwa ni fursa pia kufika katika nchi za jirani na kufanya Biashara.”

Aidha, ameahidi kutoa fursa kwa Bodi ya Chai kwa kuiunganisha na wafanyabiashara wakubwa wa Algeria ambao pia ni wawekezaji.

Kwa upande wake, Beatrice amemhakikishia Balozi huyo utayari wa TBT katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara katika sekta ya chai kwa kuwa Tanzania inawazalishaji wakubwa wa chai bora kabisa.

Ameongeza kuwa “Bodi ya Chai itaendeleza ushirikiano na Algeria kwa kuwa ushirikiano wa kibiashara kwenye sekta hii ya chai una faida kubwa kwa wakulima, wachakataji wa wadau wa sekta hii kwa ujumla, bodi ipo tayari kupokea wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuiimarisha sekta ya chai nchini.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter